Zenj FM

Wastaafu wapumua ZSSF yarahisisha uhakiki Pemba

2 July 2025, 4:24 pm

Kaimu Mkurugenzi wa ZSSF Pemba, Msabaha Massoud Msabaha

Zoezi la uhakiki kwa wastaafu wa ZSSF hufanyika mara mbili kwa mwaka, yaani mwanzoni mwa mwezi wa Januari na mwezi wa Julai, ambapo wastaafu wote wanatakiwa kufika kuthibitisha taarifa zao ili kuendelea kupokea mafao yao kwa mujibu wa taratibu.

Na Is-haka Mohammed.

Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) umeendelea kurahisisha zoezi la uhakiki wa wastaafu wanaopokea mafao yao ya uzeeni, kwa lengo la kupunguza msongamano na kuboresha huduma kwa walengwa.
Kaimu Mkurugenzi wa ZSSF Pemba, Msabaha Massoud Msabaha, amesema maboresho hayo yanalenga kuhakikisha wastaafu wanahudumiwa kwa wakati, hasa katika kipindi hiki cha uhakiki wa mwezi Julai kinachoendelea katika ofisi za mfuko huo zilizopo Tibirinzi, Chake Chake Pemba.
Aidha amesema zoezi la uhakiki ni la muhimu kwani linasaidia kutambua uwepo wa wastaafu hai wanaostahili kupokea mafao yao, hivyo kusaidia pia kudhibiti upotevu wa fedha za umma.

Sauti ya Kaimu Mkurugenzi wa ZSSF Pemba, Msabaha Massoud Msabaha.

Kwa upande wao, baadhi ya wastaafu waliokwisha kufanyiwa uhakiki wamepongeza hatua ya ZSSF kurahisisha utaratibu huo, wakieleza kuwa huduma zimeboreshwa na zinarahisisha upatikanaji wa haki zao kwa haraka.

Sauti ya baadhi ya wazee.