Zenj FM

UWT yataka wanawake kuchukua hatua uchaguzi mkuu

28 June 2025, 9:52 pm

Makamo Mwenyekiti wa Jumuiya ya wanawake UWT Tanzania Zainab Khamis Shomar akitowa taarifa kwa waandishi wahabari katika ukumbi wa mkutano ofisi ya Chama Cha Mapindizi CCM Mkoa wa Kusini Pemba. Picha na Is-haka.

Chama cha Mapinduzi CCM kimeanza mchakato wa utoaji fomu za kuwania nafasi mbali mbali kupitia kura za maoni ndani ya chama .

Na Is-haka Mohamed
Makamo Mwenyekiti wa Jumuiya ya wanawake UWT Tanzania Zainab Khamis Shomar amewataka wanawake kujitokeza kwa wingi katika uchukuwaji wa fomu za kuwania nafasi mbali mbali kwenye majimbo yao.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mkutano ofisi ya Chama Cha Mapindizi CCM Mkoa wa Kusini Pemba zilizopo Chachani Chake Chake.

Amesema ili kufikia uwakilishi wa 50/50 kwa wanawake katika vyombo vya kutoa maamuzi wakati umefika wa kuchukua fomu za kuwania nafasi hizo,huku akiwataka wapiga kura wanawake katika vyama mbali mbali kuwaunga mkono wagombea wanawake.

Aidha amesema nia yao nikumuona Mama Samia arudi tena kuliongoza taifa la watazania kwani katika uongozi wake amekuwa akionesha upendo,uwaminifu na uzalendo wa kutosha kwa wananchi
wake.

Sauti ya Makamo Mwenyeti wa Jumuya ya wanawake UWT Tanzania Zainab Khamis Shomar.