Zenj FM

Dkt. Mwinyi aimarisha huduma za kijamii Zanzibar

4 June 2025, 1:18 pm

Katibu wa Idara ya Itikadi, uenezi na mafunzo wa Chama cha Mapinduzi Khamis Mbeto Khamis.

Na Mwandishi wetu.

Huduma za afya , Miundo mbinu na elimu zimehimalika kwa kiwango kikubwa katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais wa Zanzibar Dk Hussen Ali Mwinyi.

Katibu wa Idara ya Itikadi, uenezi na mafunzo wa Chama cha Mapinduzi Khamis Mbeto Khamis ameyasema hayo alipokuwa akizungumzia utekelezaji wa Ilana ya uchaguzi ya mwaka 2025.

Sauti ya Katibu wa Idara ya Itikadi, uenezi na mafunzo wa Chama cha Mapinduzi Khamis Mbeto Khamis,

Aidha amesema Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan amefanya kazi kubwa ya kuendelea kukamilisha miradi mikakati ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa Bwawa la umeme la Mwalimu Nyerere, Reli ya tireni ya mwendo kasi (SGR) na daraja la kwanza kwa urefu Afika mashariki la busisi mkoa wa Mwanza.

Sauti ya Katibu wa Idara ya Itikadi, uenezi na mafunzo wa Chama cha Mapinduzi Khamis Mbeto Khamis,

Uchaguzi Mkuu wa Rais wa Zanzibar na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unatarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu, ambapo Rais Samia na Dk. Mwinyi tayari wamechaguliwa kuwa wagombea wa urais wa Muungano na Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM.