Zenj FM

Timu ya 34 ya madaktari wa China yatoa huduma za afya kwa watoto Mazizini

2 June 2025, 6:44 pm

Kingozi wa Madaktari wa timu ya 34 kutoka China Dkt Wei Chen, akiwapatia huduma ya afya watoto yatima Mazizini.

Na Omary

TIMU ya 34 ya Madaktari kutoka China wamewafanyia uchunguzi na kupatiwa
huduma za afya watoto wanaolelewa katika kituo cha kulelea watoto Mayatima
Mazizini.
Akizungumza mara baada ya kuwapatia huduma watoto hao Kingozi wa
Madaktari wa timu ya 34 kutoka China Dkt Wei Chen amesema jumla ya watoto
60 wamepatiwa huduma na wataendelea kuisaidia sekta ya Afya katika nyanja
tofauti ikiwemo kuwapatia huduma wananchi wa visiwa vya Unguja na Pemba
pamoja na watoto wenye mahitaji maalumu.
Amefahamisha kuwa watoto wanaolelewa kituo Cha Mazizini na vituo vyengine
wanahitaji kuchunguzwa afya zao mara mara kwa mara na endapoa watakuwa na
matatizo ya kiafya waweze kuhudumiwa na kuondokana na maradhi na waweze
kuishi kwa furaha katika maisha yao.
Amesema Serikali ya China itaendelea kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar katika kuimarisha huduma mbali mbali ikiwemo sekta ya Afya kwa kutoa
huduma katika maeneo mbali mbali hapa nchini, kuwajengea uwezo wataalamu
pamoja kusaidia dawa na vifaa tiba.

Sauti ya Kingozi wa Madaktari wa timu ya 34 kutoka China Dkt Wei Chen.

Kwa upande wake Mama wa Kituo cha kulelea watoto Mayatima Mazizizni
Wahida Abdalla Hassan amefurahishwa na ujio wa madaktari hao kwa
kuwahudumia watoto mayatima katika kituo hicho ambapo wamefanyiwa vipimo
na matibabu kutoka kwa madaktari hao
Aidha ameiomba timu ya madaktari hao wa kichina kuendela kuwapatia huduma
watoto hao katika kituo hicho ili kuondokana na maradhi mbali mbali.

Sauti ya Mama wa Kituo cha kulelea watoto Mayatima Mazizizni Wahida Abdalla Hassan.

Timu ya 34 ya madaktari kutoka China imekuwa na kawaida kutoa huduma na
kufanya uchunguzi wa maradhi kwa wananchi mbali mbali na makundi maalumu
kwa kuwafata katika maeneo yao.