Zenj FM
Zenj FM
2 June 2025, 1:42 pm

Na Is-haka Mohammed
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda amesema ujenzi wa Skuli ya Ufundi itakayojengwa hivi karibuni kambini kisiwani Pemba ni kuunga mkono serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika uimarishaji maendeleo ya elimu inayoendelea kuimarishwa kwa kiwango kibwa na serikali ya amwanu ya Nan echini ya Rais Dr. Hussein Ali Mwinyi
Prefesa Mkenda ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa jimbo la Kojani katika hafla la makabidhiano ya eneo la ujenzi wa Skuli ya Ufundi Kambini Kichokochwe lililokabidhiwa na mbunge wa jimbo hilo Hamad Hassan Chande itakayoanza kujengwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teklojia ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambapo jumla ya ekari kumi zimekazibiwa kwa ajili ya ujenzi wa chuo hicho .
Aidha Pro, Mkenda amesema Wizara yake itaendelea kufanyakazi kwa pamoja na Wiara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar ili kuona sekta ya elimu inaendelea kuimarika visiwani.
Akimkaribisha Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia kuzungumza na wananchi, Mbunge wa Jimbo la Kojani ambaye ni Naibu Waziri wa Fedha wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hamad Hassan Chande ujenzi wa Skuli hiyo itafungua zaidi milango ya elimu kwa vijana wa Kojani na Pemba.
Afisa Mdhamini wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Pemba Moh`d Nassor Salim ameahidi kuwa Wizara ya ya Elimu Zanzibar itakuwa karibu kutoa ushikiano wa Skuli hiyo.
Baadhi ya wazee wa Shehia ya Kambini wamesema ujenzi wa mradi huo wa Skuli ya Ufundi wameupokea kwa mikono miwili na watatoa ushirikiano kwa wajenzi.