Zenj FM
Zenj FM
7 May 2025, 6:44 pm

Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale wa Zanzibar, Mudrick Ramadhan Soraga,akisaini makubaliano ya ushirikiano kati ya wizara yake na taasisi nane muhimu za sekta ya utalii, iliyofanyika katika ukumbi wa Park Hyatt, Zanzibar.Mary Julius.
Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale wa Zanzibar, Mudrick Ramadhan Soraga, amesema kwa kuwa utalii ni sekta yenye wadau wengi, wizara yake imeamua kusimamia ushirikiano wa pamoja ili kuondoa hali ya ushindani usiokuwa na tija na badala yake kuhimiza mshikamano, upendo, na mashirikiano katika kukuza utalii wa Zanzibar.
Kauli hiyo ameitoa katika hafla ya kusaini makubaliano ya ushirikiano kati ya wizara yake na taasisi nane muhimu za sekta ya utalii, iliyofanyika katika ukumbi wa Park Hyatt, Zanzibar.
Aidha Waziri Soraga amesema makubaliano hayo yanakusudia kuimarisha sekta ya utalii ambayo kwa sasa inachangia asilimia 30 ya pato la Taifa na asilimia 70 ya mapato yote ya fedha za kigeni kwa Zanzibar pamoja na kuboresha tamasha la Maonyesho ya Utalii na Uwekezaji Zanzibar.
Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale wa Zanzibar, Mudrick Ramadhan Soraga.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wawekezaji wa Utalii Zanzibar (ZATI), Fatma Ali Mohammed.Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wawekezaji wa Utalii Zanzibar (ZATI), Fatma Ali Mohammed, amesema makubaliano haya yanalenga kujenga mshikamano wa kudumu kati ya serikali na sekta binafsi.
Aidha amesema kupitia matamasha na kampeni za pamoja, Zanzibar itaweza kuvutia watalii wengi zaidi huku ikiboresha viwango vya huduma vinavyotolewa kwa wageni wanaotembelea visiwa hivyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wawekezaji wa Utalii Zanzibar (ZATI), Fatma Ali Mohammed.Taasisi hizo zilizosaini mkataba huo ni pamoja na Kamisheni utalii Utalii Zanzibar, Jumuiya ya mahoteli Zanzibar (HAZ), Jumuiya ya wafanyabiashara Zanzibar, Jumuiya ya wawakezaji Kwenye utalii Zanzibar (ZATI), Jumuiya ya Misafara ya watalii (ZATO), Jumuiya ya watembeza watalii Zanzibar (ZATOGA), Jumuiya Ya Wawekezaji wa Nyumba za biashara (REDA) pamoja na Maonyesho ya Utalii na Uwekezaji Zanzibar.