Zenj FM

Jamii ishiriki kutokomeza malaria Zanzibar

24 April 2025, 6:43 pm

Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Afrya, Dk.Amour Suleiman wakati wa maadhimisho ya siku ya malaria yaliyofanyika Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Na Mary

Jamii imetakiwa kuendelea kuzingatia njia za kujikinga na ugonjwa wa malaria kwa kuchukua tahadhari ili kuepukana ugonjwa huo.
Wito umetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Amour Suleiman wakati wa maadhimisho ya siku ya malaria yaliyofanyika Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Amesema, kutokana na ugonjwa wa malaria kuendelea kuwepo jamii inawajibika kuzingatia usafi wa mazingira sambamba na miongozo ya wataalamu ili kuutokemeza ugonjwa huo.
Amesema, malaria ni ugonjwa wenye athari kubwa katika maendeleo ya jamii na kulingana na ripoti ya afya duniani ya mwaka 2023, wagonjwa milioni 249 na vifo 608, viliripotiwa duniani mwaka 2022.
Amesema, ingawa Zanzibar imekuwa na kiwango cha chini cha maambukizo ya malaria, mwaka 2023 wagonjwa 19, 579 waliripotiwa kuwa na malaria ambapo 1,556 kati ya hao walikuwa na laria kali na 29 walifariki.

Sauti yaMkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Afrya, Dk.Amour Suleiman.

Kwa upande wake Meneja wa Kitengo cha Kumaliza Malaria Zanzibar, Shija Joseph Shija, amesema, hali ya malaria mwaka huu imepungua kwa asilimia 43 ikilinganishwa na hali ya mwaka jana ambapo jumla ya wagonjwa 3,741 waliripotiwa kutoka Januari hadi Aprili ikilinganishwa na wagonjwa 11,418 katika kipindi kama hicho mwaka jana.

Amezitaja wilaya zinazoongoza kuripoti wagonja wengi ni wa malaria ni Mjini ikitoa asilimia 22 ya wagonjwa, Magharibi ‘B’ asilimia 20 na Magahribi ‘A’ asilimia 15 kwa Zanzibar nzima

Sauti ya Kitengo cha Kumaliza Malaria Zanzibar, Shija Joseph Shija.