Zenj FM

Soko la Mwanakwerekwe lavamiwa na wizi wa honda

16 April 2025, 5:31 pm

Mkuu wa Wilaya ya Magharibi B Hamida Mussa Khamis akiwa katika soko la Mwanakwerekwe.

Na Mary Julius.

Wafanyabiashara wa Soko la Mwanakwerekwe wameiomba Serikali kumsimamia muwekezaji wa Soko hilo kuimarisha ulinzi na Usalama wa vyombo vyao katika maeneo ya maegesho ili kuweza kufanya biashara bila ya kuwa wa wasiwasi wa usalama wa vyombo vyao.
Wakizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Magharibi B katika Soko la Mwanakwerekwe wamesema kumetokea matukio ya kuibiwa Honda za wafanyabiashara na wanunuzi wanaokuja katika soko hilo hivyo wameomba kuwekewa utaratibu ambao utawezesha vyombo vyao kuwa salama vinapokuwa katika maegesho.
Aidha wameomba kuongezwa kwa kamera katika maeneo ambayo yanayoegeshwa vyombo mara kwa mara pamoja na kuweka kadi maalum pale wanapoegesha vyombo vyao katika soko hilo.

Sauti ya wafanyabiashara.

Mkuu wa Wilaya ya Magharibi B Hamida Mussa Khamis amewaomba wafanyabiashara wa soko hilo kuendelea na Biashara zao na Tayari Serikali imeshatoa maelekezo kwa muekezaji njia sahihi ya kuweza kuimarisha usalama wa vyombo pindi wafanyabiashara na wanunuzi wanapoingia katika soko hilo.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Magharibi B Hamida Mussa Khamis.

Kwa Upande wake Mkuu wa Soko la Mwanakwerekwe Sharifu Ali Sharifu na Meneja Operesheni Soko hilo Mundhiri Abdalla Humudi na wamesema kwa kipindi cha hivi karibuni takribani matukio manne yamejitokeza ya kuibiwa Honda aina ya Click katika maeneo ya maegesho na kufanikiwa kumkamata mtu mmoja akiwa katika jaribio la kuiba.

Sauti ya Mkuu wa Soko la Mwanakwerekwe Sharifu Ali Sharifu na Meneja Operesheni Soko hilo Mundhiri Abdalla Humudi.