Zenj FM

Makini: Wanawake, wenye ulemavu kugombea bila gharama

16 April 2025, 4:09 pm

Katibu Mkuu Taifa wa chama cha Makini, Amier Hassan Ameir.

Na Mary Julius.

Katika kuhakikisha wanawake na watu wenye ulemavu wanashiriki kamilifu katika kuwania nafasi za uongozi katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, Chama cha Makini kimetangaza kutoa fomu bure kwa watia nia wanawake na watu wenye ulemavu watakaotaka kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kupitia chama hicho.
Akizungumza na Zenji FM, Katibu Mkuu Taifa wa chama cha Makini, Amier Hassan Ameir, amesema hatua hiyo inalenga kuwawezesha wanawake na watu wenye ulemavu kushiriki kikamilifu katika mchakato wa uchaguzi kwa kuondoa changamoto za kifedha zinazoweza kuwazuia kugombea.
Aidha, Katibu Mkuu huyo amesema chama hicho kimejipanga kushiriki kikamilifu katika uchaguzi huo katika ngazi zote, kuanzia Urais, Ubunge, Uwakilishi hadi Udiwani.
Amewahimiza wanachama wote wenye sifa kuchukua fomu za kugombea mapema na kujiandaa kwa uchaguzi kwa nidhamu na uwajibikaji.

Sauti ya Katibu Mkuu Taifa wa chama cha Makini, Amier Hassan Ameir.

.Aidha, akizungumzia kuhusu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Katibu Mkuu Amier Hassan Ameir ameelezea kusikitishwa kwake na maamuzi ya chama hicho ya kukataa kusaini , akisema kuwa hatua hiyo inaweza kudhoofisha juhudi za pamoja za kuhakikisha uchaguzi huru, wa haki na wenye ushirikishwaji.

Sauti ya Katibu Mkuu Taifa wa chama cha Makini, Amier Hassan Ameir.