Zenj FM

Marhabaa Zanzibar yainogesha Halotel

14 April 2025, 3:15 pm

Balozi wa kampeni ya Marhaba Zanzibar, Jamila Abdalla,(Baby J) akiwa katika jukwaa la Marhabaa concert lililofanyika katika viwanja vya Mapinduzi Square.

Na Mary Julius.

Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Halotel, Roxana Kadio, amesema kampuni hiyo imejikita katika kuhakikisha wateja wake wanapata huduma bora, kwa kuwajali watumiaji wa mtandao huo hususan waliopo Zanzibar.
Akizungumza katika tamasha la muendelezo wa uzinduzi wa kampeni ya Marhaba Zanzibar, Roxana amesema kampeni hiyo maalum imebuniwa mahsusi kwa ajili ya wateja wa Zanzibar na inapatikana katika visiwa hivyo pekee.
Aidha Roxana amesema Katika kampeni ya Marhabaa Zanzibar , Halotel inatoa huduma mbalimbali za ofa zitakazowawezesha wateja wake kufurahia mawasiliano , bei nafuu, na huduma za kisasa zinazokidhi mahitaji ya kila siku.

Sauti ya Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Halotel, Roxana Kadio.

Kwa upande wake, Balozi wa kampeni ya Marhaba Zanzibar, Jamila Abdalla,(Baby J) ameeleza kufurahishwa kwake na uzinduzi wa kampeni hiyo, ambapo amesema imekuja wakati muafaka.
Aidha amesema wamechaguliwa kuwa mabalozi wa Marhabaa Zanzibar kwa sababu wana ushawishi miongoni mwa vijana na jamii na ameahidi kuyatumia majina yao kufikisha ujumbe kwa watu wa Zanzibar ili kuvunja mipaka ya mawasiliano.

Sauti ya Balozi wa kampeni ya Marhaba Zanzibar, Jamila Abdalla,(Baby J).

Kampeni ya Marhaba Zanzibar inalenga kuongeza upatikanaji wa huduma za mawasiliano , kuwapa wateja ofa maalum, na kuwaunganisha Wazanzibari ambapo katika tamasha hilo lililo fanyika katika viwanja vya Mapinduzi square wasinii mbalimbali walipanda jukwaani ikiwemo Baby J, Berry black na wengine wengi.