Zenj FM

Ziara ya Dkt. Mwinyi Uingereza neema kwa wakulima wa mwani Zanzibar

11 April 2025, 3:32 pm

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt, Hussein Ali Mwinyi amesema Wawekezaji wengi wa Uingereza.

Na Mary Julius.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt, Hussein Ali Mwinyi amesema Wawekezaji wengi wa Uingereza wameonesha nia ya kuwekeza katika Kuliongezea thamani zao la Mwani kwa kuongeza Mnyororo wa Thamani pamoja na Uzalishaji wa Mbegu Bora.
Rais Dkt,Mwinyi amesema hayo alipozungumza na Waandishi wa Habari Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Baada ya Kuwasili Nchini akitokea Uingereza alikohudhuria Mkutano wa Jumuiya ya Madola wa Masuala ya Biashara na Uwekezaji uliojikita katika Agenda ya Uchumi wa Buluu.
Rais Dkt, Mwinyi amezitaja Sekta Tatu kuu za Uchumi ikiwemo Utalii,Uchumi wa Buluu na Utafutaji wa Mafuta na Gesi ndio Sekta za Kipaumbele kwa Serikali ambazo Wawekezaji wengi wamedhamiria kuwekeza na Serikali imewahakikishia Ushirikiano kufanikisha Azma zao.
Akizungumzia Sekta ya Mafuta na Gesi amesema Kampuni nyingi zimejitokeza ambazo zimeingia Mkataba na Serikali Juu ya Utafutaji wa Data za Mafuta na Gesi na Kuzitangaza Duniani kwa ajili ya Kupata Wawekezaji Zaidi.

Sauti ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt, Hussein Ali Mwinyi.

Aidha Rais Dkt,Mwinyi amewahakikishia Wawekezaji kuwa Zanzibar bado Ina fursa nyingi za Uwekezaji na kukuza Uchumi na Serikali inazitangaza kwa Kiwango kikubwa.