

26 March 2025, 4:43 pm
Na Thuwaiba Mohammed.
Madiwani wa Wiaya ya Magharib B wametakiwa kuwa mabalozi kwa wananchi katika wadi zao juu ya matumizi na faida za utumiaji wa Mfuko wa Huduma za Afya Zanzibar ZHSF.
Mstahiki Meya wa Baraza la Manispaa ya Wilaya ya Magharib B Khamis Hassan Haji ametoa kauli hiyo baada ya mafunzo kwa madiwani kutoka mfuko wa huduma za afya Zanzibar yalofanyika Baraza la Manispaa ya Magharib B Wilaya ya Maghari B Unguja.
Meya amemshukuru Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi kwa kuhakikisha wananchi wa Zanzibar wanapata huduma bora ya afya kwa kutumia mfuko huo.
Akitoa mada na historia ya mfuko huo katika mafunzo hayo Meneja kitengo cha tathmin ya uhimilivu na usimamizi kutoka mfuko wa huduma za afya Abdul Majid Kareem amesema malengo ya mfuko huo ni kuhakikisha upatikanaji bora wa huduma za afya na zenye uhakika kwa wananchi na wakaazi wa Zanzibar.
Wakizungumza kwa niaba ya Madiwani wa Wilaya hiyo Mwenyekiti wa Madiwani wa Wilaya ya Magharib B na Diwani wa Wadi ya Pangawe Mwan jaha Nahoda pamoja na Diwani wa kuteuliwa Nassor Amir Nassor wameahidi kuwa mabalozi kwa wananchi kwa kuwapeleka elimu hiyo ya umuhimu wa mfuko wa huduma za Afya Zanzibar na wameutaka mfuko huo kuandaa utaratibu wa kuhakikisha wanawafikia wananchi kuwapa elimu hiyo ili kufikia lengo la serikali la kutoa huduma bora za afya kwa wananchi wake.