

24 March 2025, 3:55 pm
Na Mwandishi wetu.
Mwanasiasa mkongwe na mbunge wa zamani jimbo la Kikwajuni Parmukh Singh Hoogan amesema sio muafaka kiongozi kutoa sadaka kwa dhehebu moja la dini na kuacha mengine wakati wewe kiongozi wa Taifa.
Singh amesema alipokuwa akizungumzia tatizo la rushwa ya uchaguzi na utaratibu wa utoaji wa sadaka unaofanywa na wanasiasa kwa wanannchi.
Akizungumzia umasikini Singh amesema wanaosema uchumi umekuwa washuke chini wajionee maisha wanayoishi watu wa chini.
Aidha amesema wanataaluma wengi nchini sasa wanakimbia kazi za taaluma zao na kuingia katika siasa kutokana na kulipwa maslahi duni jambo ambalo hatari kwa maendeleo ya Taifa.
Akizungumzia tatizo la ukosefu wa huduma ya maji safi ya uhakika amesema wakati umefika Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) kuvunjwa na kuundwa upya wapatikane watendaji wenye uwezo.
Mwanasiasa mkongwe Parmukh Singh Hoogan amekuwa mjadala mkubwa visiwani Zanzibar kutokana na misimamo yake yakutetea misingi ya demokrasia na utawala bora.