

23 March 2025, 4:53 pm
Na Khamis
BENKI ya Watu wa Zanzibar (PBZ) kwa kushirikiana na Taasisi ya Asma Mwinyi Foundation imewapatia msaada wa vitu mbalimbali wananchi wakiwemo, mayatima, wajane, wazee na watu wenye mahitaji maalum wa shehia ya Muyuni ‘C’.
Akizungumza mara baada ya kuwapatia msaada huo, Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Taasisi ya Asma Mwinyi Foundation, Asma Ali Hassan Mwinyi, amesema, benki hiyo imekuwa na utaratibu wa kutoa msaada kwa watu na makundi mbalimbali hususani kipindi hiki cha mfungo wa mwezi mtukufu wa ramadhani.
Amesema taasisi ya Asma Mwinyi Foundation itaendelea kuwahamasisha wadau wengine mbalimbali kuona wananchi wanaohitaji wanapata misaada kama hiyo katika shehia nyengine.
Kwa upande wake Sheha wa shehia ya Muyuni ‘C’, Hassan Amour Ali, amesema, maamuzi ya taasisi ya Asma Mwinyi Foundation kufika katika shehia hiyo, kwa kuwapatia msaada makundi hayo, yameleta faraja kubwa kwani katika shehia kumekuwa na wengi wenye uhitaji wa misaada kama hiyo.
Nao baadhi ya waliopatiwa msaada huo Ali Mohamed Ali, na Amina Nahodha Makame wameshukuru kupatiwa msaada huo na kuahidi kutumia kama ilivyokusudiwa na pamoja na kuwaomba wadau mbali mbali kuendelea kusaidi makundi maalum ya watu wenye uhitaji.
Zaid ya Familia 60 wa shehia ya Muyuni ‘C’, wamepatiwa msaada ikiwemo sukari, unga wa ngano, mafuta ya kula na mchele.