Zenj FM

Kadhi Mkuu Zanzibar, waumini wa Chumbuni waombea viongozi

23 March 2025, 4:27 pm

Kadhi mkuu wa Zanzibar Sheikh Hassan Othman Ngwali akizungumza baada ya kumaliza Dua Maalumu ya Kuwaombea viongozi wa kitaifa Katika Msikiti wa Ijumaa Bamita Sheikha Hassan.

Na Mary Julius.

Kadhi mkuu wa Zanzibar Sheikh Hassan Othman Ngwali ameungana na waumini wa Dini ya Kiislam wa Jimbo la Chumbuni katika Dua Maalumu ya Kuwaombea viongozi wa kitaifa na wa Jimbo hilo ili waendelee kutekeleza vyema majukumu yao katika kuwaletea maendeleo wananchi.
Akizungumza baada ya kumaliza Dua hiyo Katika Msikiti wa Ijumaa Bamita Sheikha Hassan amesema kufanya hivyo ni sehemu ya kuunga Mkono juhudi zinazochukuliwa na viongozi mbalimbali nchini ambazo zimekuwa zikibadilisha mwenendo wa Zanzibar pamoja na wananchi wake.
Aidha amesema ni nyema wananchi wa maeneo mbali mbali kuendeleza amani iliyopo katika nchi pamoja na kuwa na utamaduni wa kuwaombea viongozi na kuiombea nchi iendelee kuwa na utulivu.

Sauti ya Kadhi mkuu wa Zanzibar Sheikh Hassan Othman Ngwali.

Nae Kaimu Amiri Jumuiya ya maimamu Zanzibar JUMAZA Wilaya ya Mjini Sheikh Rashid Juma Soud amesema jumuiya ya imamu inaunga mkono dua kama hizo za kuwaombea viongozi pamoja na kuiyomba misikiti mengine kuiga mfano wa kuomba dua kama hizo.

Sauti ya Kaimu Amiri Jumuiya ya maimamu Zanzibar JUMAZA Wilaya ya Mjini Sheikh Rashid Juma Soud.

Akizungumza kwa Niaba ya Mbuge wa Jimbo la Chumbuni Murtaz Saleh Mbaraka amesema ofisi ya mbunge iko pamoja na wananchi katika kushirikia kufanya dua za kuiyombea nchi na viongozi katika miskiti mbali mbali iliyomo katika jimbo hilo.