Zenj FM

Mwakilishi wa Malindi aahidi chakula wanafunzi kidato cha sita

22 March 2025, 5:07 pm

Baadhi ya waalikwa katika futari iliyo andaliwa na skuli ya sekondari ya Kiponda.

Na Mary Julius.

Mwakilishi wa Jimbo la Malindi Mohamed Ahmada Salum ameahidi kutoa chakula kwa skuli zote zilizopo katika jimbo hilo kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha sita wanakuwa kambini kwa maandalizi ya mitihani.

Mwakilishi Ahmada ameyasema hayo katika futari iliyo andaliwa na skuli ya sekondari ya kiponda kwa ajili ya wananfunzi na walimu,amesema anafanya hivyo ili kuwawezesha wanafunzi kusoma kwa bidiii na kuja na matokeo mazuri katika mitihani yao.

Aidha Ahadi ya kuendelea kushirikiana na skuli zote hata baada ya kumaliza majukumu yake kama mwakilishi.

Sauti ya Mwakilishi wa Jimbo la Malindi Mohamed Ahmada Salum.

Kwa upande wake Afisa Sekondari Mwalimu Haroub Ali Hamadi amempongeza mwakilishi kwa juhudi mbalimbali anazozushukua katika kuendeleza elimu katika jimbo hilo.

Sauti ya Afisa Sekondari Mwalimu Haroub Ali Hamadi.

Nae Kaimu Mwalimu Mkuu wa skuli ya Sekondari ya Kiponda Miza Kai Khamis amesema wameandaa futari hiyo ili kuwafanya vijana wajisikie faraja na kuwapa nguvu na motisha ya kusoma kwa bidii.

Aidha amewataka wazazi na jamii kuwa karibu katika kuwasaidia watoto waliopo kwenye makambi ili wapate mwamko wa kusoma kwa bidii na hatimaye kupata matokeo mazuri.

Sauti ya Kaimu Mwalimu Mkuu wa skuli ya Sekondari ya Kiponda Miza Kai Khamis.

Wakizungumza kwa niaba ya wanafunzi wa kidato cha sita wanafunzi wameahidi kusoma kwa bidii na kuwaomba wanafunzi wenzao kuamka na kupambania maono yao kwani siku ni chache zilizo baki.

Aidha wameupongeza uongozi wa skuli na Mwakilishi wa Jimbo la Malindi kwa kuwanandalia futari hiyo ambayo imewapa faraja na kujisikia kama wapo nyumbani.

Sauti ya wanafunzi.