Zenj FM

Walimu Wilaya ya Kati wahimizwa kufanya tathmini mara kwa mara

21 March 2025, 5:23 pm

Afisa Taaluma Sekondari Wilaya ya Kati Hamdu Zubeir Ameir ( alievalia kofia ya Kiua ) akisikiliza kwa makini Changamoto mbali mbali, maoni na ushauri kutoka kwa Walimu Wakuu wa Skuli za Sekondari za Serikali na Binafsi za Wilaya ya Kati.

Wilaya ya Kati.

Walimu wanatakiwa kufanya tathmin mara kwa mara ili kufahamu wapi kuna Changamoto ili kuweza kuzitatua Changamoto hizo mapema kabla ya kufika muda wa kufanya mitihani ya Taifa.

Hayo ameyasema Afisa Taaluma Sekondari Wilaya ya Kati HAMDU ZUBEIR AMEIR katika mkutano wa kutahmini matokeo ya kidato cha pili na kidato cha nne kwa mwaka 2024 hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Afisi ya Elimu Kidimni Wilayani humo.

Amesema kila mwalimu anatakiwa kujitathmini katika masomo yake anayoyasomesha kila mwezi ili kufaham wapi kunachangamoto kwalengo la kuongeza ufaulu maskulini.

Kwa upande wake Afisa Tehama Mwalim Mohammed Masoud Mohammed amewaomba Walimu Wakuu na Walimu wa Taaluma kushirikiana kwa pamoja na kuhakikisha wanafanya Tathmini kila baada ya muda ili kufikia lililokusudiwa.

Sauti ya Afisa Tehama Mwalimu Mohammed Masoud Mohammed.

Nae Mkuu wa Taaluma kutoka Skuli ya Tunguu Sekondari Mwanaisha Ahmada Mohammed amesema Skuli hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kukosekana kwa muda wa Masomo ya ziada kwa Wanafunzi jambo ambalo linapelekea kutomaliza Silibasi kwa wakati.

Sauti ya Mkuu wa Taaluma kutoka Skuli ya Tunguu Sekondari Mwanaisha Ahmada Mohammed.

Nao baadhi ya Walimu ya Wakuu kutoka Skuli mbalimbali walioshiriki katika Mkutano huo wamewaomba Walimu wenzao kuyatekeleza yale yote yaliojadiliwa katika Mkutano huo kwalengo la kuongeza ufaulu katika Mkoa wao.

Sauti za Walimu.

Jumla ya Walimu 60 wa Skuli za Sekondari za Serikali na Binafsi za Wilaya ya Kati wameshiriki katika Mkutano huko wa Tathmini kwa Matokeo ya Wanafunzi wa Sekondari 2024.