

21 March 2025, 4:28 pm
Na Berema Nassor.
Wandishi wa habari visiwani Zanzibar wametakiwa kutumia kalamu zao vizuri katika kuwahamasisha wanawake kushiriki nafasi mbali mbali za uongozi.
Mwenyekiti wa Bodi ya TAMWA Zanzibar Asha Abdi ameyasema hayo wakati wakiadhimisha siku ya wanawake duniani huko katika ukumbi Tamwa Zanzibar uliopo Tunguu wilaya ya Kati.
Amesema historia inaonesha wanawake walikuwa nyuma sana hususan katika Nyanja za nafasi za uongozi hivyo wakati umefika sasa kuweza kuwainua wanawake katika kila hatua ikiwemo nafasi za uongozi na kiuchumi.
Kwa upande wake Afisa Programme wa Mradi wa Michezo kwa Maendeleo Khairat Haji amesema lengo kuu la maadhimisho hayo ni kuangalia nafasi za wanawake katika uongozi katika michezo ni kwa namna gani wanawake wanaweza kushika nafasi mbalimbali katika sekta hiyo.
Nao baadhi ya washiriki katika maadhimisho hayo wamesema wanawake wana haki ya kupata nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya nchi na njee ya nchi sambamba na kuweza kushirikiana katika kufikia ndoto zao.
Siku yawanawake duniani huadhimishwa kila ifikapo tarehe 8 march ambapo kwa upande wa Tamwa Zanzibar wameiaadhimisha siku hiyo, kauli mbiu ya mwaka huu ni Ushiriki wa wanawake na msichana ni kichoceo cha maendeleo.