Zenj FM

Zoezi la uandikishaji wapiga kura awamu ya pili lakamilika kwa mafanikio

17 March 2025, 7:04 pm

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Jaji George Joseph Kazi Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukamilisha zoezi la kutembelea vituo.

Na Mary Julius.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Jaji George Joseph Kazi amesema zoezi la uandikishaji wa wapiga kura wapya kwa awamu ya pili limekamilika kwa mafanikio katika mikoa yote ya zanzibar.

Mwenyekiti ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukamilisha zoezi la kutembelea vituo huko Ofisini Maisara Wilaya ya Mjini,amesema zoezi la uandikishaji katika wilaya zote limefanyika kwa amani na utulivu na wananchi wamejitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari hilo ili kupata haki yao ya kidemokrasia.

Akizungumzia kuhusu kupotea kwa kitambulisho ama kuhamisha taarifa za mpiga kura Jaji Kazi amesema kuwa mwananchi afike katika Ofisi ya Tume ya Wilaya husika ili kutafitiwa ufumbuzi.

Sauti ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Jaji George Joseph Kazi .

Nao Wakuu na Mawakala wa Vituo ya wilaya ya mjini wamesema siku zote za uandikishaji zoezi limekwenda vizuri vituo vimefunguliwa kwa wakati na wananchi wamepata huduma bila ya usumbufu kila mwenye sifa ameweza kuandikishwa katika daftari la kudumu la wapiga kura.