

17 March 2025, 5:46 pm
Na Mwandishi wetu.
Mwanasiasa mkongwe na Mbunge wa zamani Parmkh Sing Hoogan amesema wakati umefika wabunge na wawakilishi waliokaa muda mrefu katika majimbo wawekewe ukomo kama wale wa Viti maalum.
Singh amesema hayo baada ya Halimashauri Kuu ya CCM kuweka ukomo wagombe viti maalum mwisho vipindi viwili kuanzia mwaka 2030.
Singh amesema muda wa vipindi viwili kuajengea uwezo wabunge na Wawakilishi katika kuwajengea uweziwa kugombea jimbo.
Amesema mifumo yote ya kugombea nafasi za uongozi mizuri kama takrima na rushwa ya uchaguzi iktadhibitiwa.
Aidha amesema wanawake wameonyesha uwezo mkubwa katika mambo ya uongozi na kutoa mfano Rais wa serikali ya Jamhuri ya muungano Dk Samia Suluhu Hassan .
Suala la kuweka ukomo wa kugombea viti maalum limeibua mjadala mkubwa baada ya kutokuwausisha wabunge waliokaa muda mrefu katika majimbo Zanzibar na Tanzania Bara.