Zenj FM

Tanzania kuwa mwenyeji mkutano mkuu wa kimataifa wa ushuru, forodha

10 March 2025, 4:17 pm

Waziri wa Uchukuzi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Prof. Makame Mnyaa Mbarawa akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Mikutano Hoteli ya Golden Tulip.

Na Mary Julius.

Waziri wa Uchukuzi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Prof. Makame M. Mbarawa amesema Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania imechaguliwa kuwa mwenyeji wa Mkutano mkuu wa Kimataifa wa Shirikisho la vyama vya Mawakala wa Ushuru na Forodha unaotarajiwa kufanyika April 30 hadi Mei 1,
Prof Mbarawa ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Mikutano Hoteli ya Golden Tulip amesama mkutano huo ambao hufanyika kila mwaka kwa kuleta pamoja wadau wa tasnia ya lojistik na usafirishaji kwa ajili ya kujadili changamoto na ushirikiano katika sekta ya uchukuzi.
Amesema Mkutano huo utashirikisha washiriki zaidi ya 500 kutoka nchi za Kimataifa kwa upande Afrika na Mashariki ya kati wakiwemo wataalamu wa usafirishaji wa lojistiki, watunga sera, wataalamu wa uwezeshaji biashara, mamlaka za udhibiti, mamlaka za bandari, wasafirishaji mizigo, watafiti na wabunifu wa sekta hizo Duniani.
Aidha Amesema lengo la Mkutano huo kubadilishana maarifa kwa kufanya majadiliano juu ya mbinu bora na utafiti wa kisasa kuhusu vifaa endelevu vya kutumia teknolojia ya kisasa pamoja na kukuza ushirikiano wa kati ya watoa huduma za vifaa, mamlaka za udhibiti wa uzalishaji, wauzaji wa rejereje na kampuni za teknolojia.

Sauti ya Waziri wa Uchukuzi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Prof. Makame Mnyaa Mbarawa.

Kwa upande wake rais wa Chama cha Mawakala wa Ushuru na Forodha Tanzania Edward Urio ameishukuru serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kukubali kuwa mwenyeji wa mkutano wa kimataifa wa shirikisho la vyama vya mawakala wa forodha wa kimataifa kwa upande wa africa na mashariki ya kati.
Aidha Edward amesema wamejipanga kupokea washiriki kutoka sehemu mbalimbali duniani ,kufanyika kwa mkutano huo hapa Zanzibar kutaongeza biashara na utalii.

Sauti ya Rais wa Chama cha Mawakala wa Ushuru na Forodha Tanzania Edward Urio .

Mgeni rasmi katika mkutano huo utakao fanyika Zanzibar anatarajiwa kuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan ukiwa na kauli mbiu ya ushirikiano katika uchumi wa buluu kubadilisha lojistiki na uchumi kwa uendelevu.