

8 March 2025, 6:47 pm
Na Kulwa Suleiman
Wafanyabiashara wa soko la Kibanda Maiti wameiomba serikali kutengeneza miundo mbinu ya soko hilo ili kuzuia maji kutuwama katika maeneo ya biashara.
Wafanyabiashara wameyasema hayo walipo zungumzana na zenji fm wamesema miundo mbinu ya soko hilo si rafiki hasa katika kipindi hichi ambacho kunatarajiwa kunyesha mvua za masika, wamesema kutuwama kwa maji kutapelekea kutofanyika kwa biashara katika soko hilo.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Baraza la Manispaa Mjini Amina Simai Msaraka amesema ujenzi wa barabara na mitaro katika maeneo ya kibanda maiti ndio sababu kubwa inayopelekea kutuwama kwa maji katika maeneo hayo ya soko.
Kaimu Mkurugenzi amewataka wafanyabiashara kuwa na subra hasa katika kipindi hichi ambacho serikali inafanya ukarabati wa miundo mbinu ya barabara na amesema baraza hilo litatumia magari ya kunyonya maji yalio tuama katika maeneo ya soko hilo.
Aidha amewaomba wafanya biashara wa eneo hilo kufanya usafi na kutotupa taka ovyo za masalia ya matunda ili kuweka mazingira ya soko katika hali ya usafi.