

6 February 2025, 4:04 pm
Na Mary Julius
Familiya moja inayoishi Chaani Mcheza shauri Mkao wa Kaskazini Unguja imewaomba Mbunge , Mwakilishi na wananchi kuwasaidia msaada wa matibabu na pempasi kwa ajili ya mtoto wao mwenye umri wa miaka nane ambaye anamatatizo ya kutoka haja ndogo na kubwa bila kizuizi.
Akizungumza na Zenjfm mama mzazi wa mtoto huyo mwenye tatizo la mgongo wazi ambalo limesababisha kukosa hisia na kutokwa na haja ndogo na kubwa tatizo ambalo limesababisha mtoto huyo kutengwa na watoto wenzie kutomuanzisha skuli.
Aidha mama mzazi amesema kwa mwaka huu wa masomo familiya hiyo imeamua kumuandikisha mtoto shule na kuiomba jamii kuwasaidia katika kuhakikisha mtoto hiyo anapata pempasi kwa ajili ya kumuhifadhi ili aendelee na masomo.
Akizungumza mtoto huyo mwenye miaka nane kwa sasa amemuomba Rais wa Jamuhiri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kumsaidia kupata matibabu ya tatizo lake na pempasi ili aweze kuendelea na masomo yake.
Kwa upande wake Mfuatialiaji wa watoto wenye ulemavu mkoa wa Kaskazini Unguja kutoka Umoja wa Watu Wenye Ulemavu Zanzibar UWZ Djuma Ali ameiomba serikali, na watu wenye uwezo kumsaidia mtoto hiyo ili ameweze kupata matibabu pamoja na pempas ili aweze kujiendeleza kielimu.
Mfuatialiaji wa watoto wenye ulemavu mkoa wa Kaskazini Unguja