

3 February 2025, 4:46 pm
Wilaya ya Kati.
Baraza la Mji Kati limefanikiwa kukusanya Jumla ya Shilingi Milioni 400, Sitini na mbili elfu, laki Moja na Saba, Mia nne na 93 sawa asilimia 100.1 4 za makusanyo ya ndani ya baraza hilo kwa mwaka 2024/2025.
Mkurugenzi wa Baraza la Mji Kati Salum Mohammed Abubakar ameyasema hayo wakati akitoa taarifa ya bajeti ya makusanyo na matumizi ya kota ya tatu pamoja na kuangalia mafanikio na changamoto ya kota ya pili ambayo imemalizika mwezi wa 12, halfa iliyofanyika katika Ukumbi wa Baraza hilo Dunga wilaya ya Kati.
Amesema Baraza hilo linaendelea na utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo katika maeneo mbalimbali ya Wilaya hiyo ili kuhakikisha Miradi hiyo inakamikika kwa wakati kama ilivyopangwa kwa maslahi ya Wananchi na Jamii kiujumla.
Kwa upande wake Afisa Mipango Baraza la Mji Kati Mauwa Juma Mussa ameeleza sababu za kuvuka kwa malengo hayo ni kutokana na utolewaji wa elimu kwa walipakodi kupitia Vyombo vya habari pamoja utoaji wa elimu ya moja kwamoja kupitia Maafisa Mapato.
Nae Mwenyekiti wa Baraza la Mji Kati Said Hassan Shaaban amewataka wakandarasi waliokabidhiwa Miradi hiyo kuikamilisha kwa wakati ili lengo la Serikali liweze kufikiwa.
Aidha Said amewaomba wananchi kulipa kodi kwa hiari,na kuthamini juhudi zinazochukuliwa na Serikali kwamaendeleo ya Taifa.