Zenj FM

Mratibu wa Vikoba Unguja amewataka wanavikundi kurejesha mikopo kwa wakati

3 February 2025, 4:17 pm

Wanakikundi wa St Joseph Mama’s katiaka picha ya pamoja.

Na Mary Julius.

Mratibu wa vikoba unguja Catherine Ifanda amewataka wanawake waliopo katika vikundi kuhakikisha wanakopa mikopo kwa malengo ya kufanya maendeleo katika jamii.
Mratibu ameyasema hayo katika ziara ya matembezi iliyo andaliwa na kikundi cha kikoba cha St Joseph mama’s huko mbwejuu mkoa wa kusini unguja, amesema wanawake wanapo kopa kwa malengo mahsusi ni njia bora ya kujiinua kiuchumi na kuimarisha familia na jamii kwa ujumla.
Amevitaka vikundi vya vikoba kuandaa Ziara za kimatembezi ambazo zinaweza kutoa fursa nzuri kwa wanavikundi kubadilisha mazingira na kupumzika kisaikolojia.
Mratibu amesema ziara hizo zinaweza kujenga afya ya akili, kwani kuwa katika mazingira mapya kunakoweza kusaidia kupunguza msongo wa mawazo na kuongeza mtazamo mpya katika maisha na kazi zao.

Sauti ya Mratibu wa vikoba unguja Catherine Ifanda.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa St.Joseph Mama’s Rose Haule amesema silaha bora ya kuendeleza katika vikundi ni upendo hivyo wanakikundi wanatakiwa kuendeleza upendo pamoja na kuzingatia ratiba ya kikundi.

Sauti ya Mwenyekiti wa kikundi cha St.Joseph mama’s.

Nae Mhasibu wa kikundi cha St Joseph mama’s Rose Kombo amewataka wanakikundi kuzingatia nidhamu ya fedha ili kuweza kujenga msingi wa mafanikio ya kifedha na kimaendeleo.
Aidha amesema changamoto kubwa katika vikoba ni marejesho hivyo amewaomba wanakikundi kuzingatia kufanya marejesho kwa wakati ili kuweza kusonga mbele na hatimaye kufikia malengo waliyo jiwekea.

Sauti ya Mhasibu wa kikundi cha St Joseph mama’s Rose Kombo.