Zenj FM

Wanawake Pemba wajitosa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi

26 January 2025, 7:02 pm

Moja kati ya maeneo yaliyoathiriwa na mabadiliko ya tabianchi na maji ya bahari kuingia katika mashamba ya wakulima huko Kambini Kichokochwe.

Na Is-haka Mohammed.

Uwepo wa uharibifu mkubwa wa mazingira katika mataifa na nchi mbali mbali duniani kunakotokana na njia tofauti kunapelekea mabadiliko ya tabianchi na moja ya athari kubwa ya Mabadiliko ya tabia nchi katika maeneo mbali mbali ni tishio kwa binadamu na viumbe hai wengine.

Miongoni mwa mambo yanayochangia mabadiliko ya tabianchi ukiondosha shughuli kubwa za viwandani pia ni masuala ya uchimbaji wa mchanga, mawe na kifusi, ukataji wa miti, na uvuvi haramu.

Mwenzetu ni Is-haka Mohammed  ametuandalia kipindi ambacho kinangalia juhudi za Kinamama wa Shehia za Kambini, Chwale na Kiuyu Minungwini katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, katika maeneo yao.

Sauti ya Is-haka Mohamed