Zenj FM

Tumieni masoko acheni kufanya biashara kando ya barabara-DC Wilaya ya Kati

24 January 2025, 7:01 pm

Mkuu wa Wilaya ya Kati Cassian Gallos Nyimbo akizungumza na wafanyabiashara wakati wa zoezi la ukaguzi wa kuangalia Wafanyabiashara ambao wanaweka biashara zao pemboni mwa barabara katika Wilaya ya Kati.

Wilaya ya Kati.

Wafanyabiashara wanaofanya biashara zao pembezoni mwa barabara wametakiwa kufuata sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa na Baraza la Mji Kati ili kufanya biashara maeneo yaliyokuwa rasmi.

Mkuu wa Wilaya ya Kati Cassian Gallos Nyimbo ameyasema hayo wakati wa zoezi la ukaguzi wa kuangalia Wafanyabiashara ambao wanaweka biashara zao pemboni mwabarabara katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Kati.
Amesema Serikali ya Awamu ya Nane imejenga Masoko ya Wajasiriamali katika kila Wilaya ili kuhakikisha inawasaidia Wananchi pia Mji unakuwa katika haiba nzuri na yakupendeza wakati wote.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Kati Cassian Gallos Nyimbo.
Mkuu wa Wilaya ya Kati Cassian Gallos Nyimbo akizungumza na wafanyabiashara wa Dunga.

Nao baadhi ya Wafanyabiashara wamesema maagizo hayo waliopewa na Mkuu wa Wilaya huyo watayafanyia kazi na kuahidi kuwa watayatumia Masoko hayo vyema pia watakuwa mabalozi wazuri kwa wengine.
Ukaguzi huo umefanyika katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo ikiwemo katika Soko la Wananchi Dunga , Dunga Mitini pembezoni mwa Barabara kwa Wauza Samaki , Matunda na Mboga mboga.