Zenj FM

Wenye ulemavu wa familia moja waomba msaada kujengewa nyumba

20 January 2025, 3:16 pm

Vijana wenye ulemavu wa viungo wa familiya ya Fumu Ali wa Chaani Mcheza Shauri

Na Mary Julius.

Jamii visiwani Zanzibar imeombwa kuisaidia familia ya Ali Fumu ya Chaani, Mcheza Shauri, Wilaya ya Kaskazini A Mkoa wa Kaskazini Unguja yenye watoto watatu wenye ulemavu wa viungo katika kuhakikisha inapata mahitaji muhimu ikiwemo nyumba ya kuishi.
Akizungumza na Zenji FM mdogo wa vijana hao Himid Ali Fumu amesema ameamua kuomba masada huo kutokana na kuelemewa na majukumu ya kuwalea kaka zake hao watatu ambao ni walemavu wa viuongo pamoja na kuilea familia yake.

Sauti ya Himid Ali Fumu.
Msingi wa nyumba iliyojengwa na Himid Ali Fumu anayo wajengea ndugu zake.

Kwa upande wake Sheha wa Chaani Mcheza Shauri Salma Khamisi Juma amekiri kuifahamu familia hiyo na kuwaomba watu wenye uwezo kuwasaidia katika kuhakikisha watu hao wanapata mahitaji yao ya msingi.

Sauti ya Sheha wa Chaani Mcheza Shauri Salma Khamisi Juma.

Naye Mfuatialiaji wa Watoto Wenye Ulemavu Mkoa wa Kaskazini Unguja kutoka Umoja wa Watu Wenye Ulemavu Zanzibar UWZ Djuma Ali amesema kutokana na mazingira wanayoishi vijana hao wenye ulemavu na hitaji lao la kuoa ameiomba serikali kuwasaidia watu hao ili waweze kupata makazi ili nao waweze kuwa na familia zao.

Sauti ya Mfuatialiaji wa Watoto Wenye Ulemavu Mkoa wa Kaskazini Unguja Djuma Ali