ZEEA yawataka wajasiriamali kusajili vikundi vyao ili kupata fursa ya mikopo
17 January 2025, 6:48 pm
Wilaya ya Kati.
Wajasiriamali wanawake wametakiwa kuzichangamkia fursa za mkopo wenye masharti nafuu kwa kuvisajili vikundi vyao ili kujiendeleza kiuchumi.
Afisa kutoka Wakala Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ZEEA Juma Maabadi Ahmed ameyasema hayo wakati akitoa mafunzo kwa wajasiiriamali huko katika ukumbi wa Baraza la Mji Kati Dunga wilaya ya Kati.
Amesema baadhi ya wajasiriamali hawafahamu lengo la kuchukua mikopo hiyo jambo ambalo linapelekea kutofikia malengo yao ya kujikwamua na hali ngumu ya kiuchumi.
Kwa upande wake Mkuu wa Divisheni wa Mapato Uchumi na Wajasiriamali Helena John Batholomeo amewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kutumia fursa hiyo ili lengo la serikali liweze kufikiwa.
Nao baadhi ya Wajasiriamali wamesema hivi sasa wanawake sio muda wa kukaa majumbani na badala yake wajiunge na vikundi hivyo ili wapate kujikomboa na hali ngumu ya kimaisha.
Aidha wajasiriamali hao wameahadi kuyafanyia kazi Mafunzo hayo na kuahidi mikopo watayapatiwa watafanyia mambo ya Maendeleo.