Zenj FM

Mtaro wa Sebleni hatari kwa watoto

19 December 2024, 4:16 pm

Hali ya Mtaro wa Sebleni.

Na Mwajuma Said Yussuf na Halsa Abdallah Juma

Wananchi wa shehia ya sebleni wilaya ya mjini wameliomba baraza la manispaa kuufunika na kuungeza kina mtaro sebeleni ili kulinda maisha ya watoto pamoja na afya za wakaazi wa eneo hilo.

Wakizungmza na zenji fm wakazi hao wamesema kuwepo wazi kwa mtaro huo kumekuwa ni sababu ya baadhi ya wananchi  kutupa taka ndani ya mtaro huo hali inayopelekea kuziba  na kumwaga maji katika maeneo ya makazi ya watu.

Aidha wamewaomba wananchi wenzao kuacha kutupa taka katika mtaro huo hasa katika kipindi cha mvua.

Sauti ya Wananchi.

Akizungumza kwa niaba ya Sheha wa Shehia hiyo  Khamis Mkanga Ali amewataka wananchi hao kuacha tabia ya kutupa taka katika mtaro huo kwa lengo la kulinda afya zao na kuwataka manispaa kutimiza wajibu wao kwa wananchi.

Sauti ya Khamis Mkanga Ali .

Kwa upande wake Afisa Mazingira Manispaa ya Mjini Rajab Iddi Abdullah awahakikishia wananchi kulishulkia suala hilo pamoja na kutoa wito  kwajamii , kutoa mashirikiano katika kuhakikisha wanadumisha usafi wa mtaro huo kwani suala la usafi wa mazingira sio la manispaa pekee bali ni suala la jamii kwa ujumla.

Sauti ya Afisa Mazingira Manispaa ya Mjini Rajab Iddi Abdullah.