Zenj FM

Tadio yawakumbusha waandishi kuzingatia maadili uchaguzi mkuu

13 December 2024, 4:04 pm

Mhariri wa Radio Tadio Hilali Alexander Ruhundwa akiwa na wafanyakazi wa Zenj FM katika mafunzo ya kuwajengea uelewa waandishi wa habari kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025.

Na Mary Julius

Waandishi wa habari wametakiwa kuzingatia maadili katika kuandika habari hasa katika kipindi cha uchanguzi mkuu ili kuikinga nchi kuingia katika machafuko.

Kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025 Radio Tadio imetoa mafunzo  kwa waandishi wa habari wa Zenj FM ili kuwajengea uwezo waandishi hao katika kuzingatia maadili katika kipindi hicho cha uchaguzi.

Akizungumza mara baada ya mafunzo hayo yaliyofanyika katika chumba cha habari cha Zenj FM Mombasa Zanzibar/, Mhariri wa Radio Tadio Hilali Alexander Ruhundwa amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwaandaa waandishi wa habari katika kuandika na kuripoti habari za uchaguzi kwa usahihi, uwazi na kwa misingi ya maadili ya habari.

Amesema mafunzo hayo yana lengo la kuhakikisha kuwa waandishi wanakuwa na uwezo wa kutoa taarifa sahihi na za uhakika wakati wa kipindi cha uchaguzi, huku wakiangalia masuala muhimu kama usawa, ufanisi na kuepuka upotoshaji wa taarifa.

Sauti ya Mhariri wa Radio Tadio Hilali Alexander Ruhundwa.

Akizungumza kwa niaba ya waandishi wa Zenji FM Berea Nassor ameishukuru radio tadio kwa kuwaandalia mafunzo hayo ambayo yatakuwa muongozo katika kuandika habari hasa katika kipindi cha uchaguzi mkuu wa 2025.

Sauti ya Mwaandishi wa Zenji Fm Berema Nassor.