Zenj FM

Wanahabari Pemba watoa wito marekebisho ya sheria za habari

11 December 2024, 3:55 pm

Afisa Programu na Uchechemuzi wa Sheria za Habari Zanzibar Kutoka Tamwa-Zanzibar Zaina Abdulla Mzee akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari huko katika ukumbi wa Tamwa Mkanjuni Pemba.
 

Na Is-haka Mohammed.

Waandishi wa Habari Kisiwani Pemba wameelezwa kutochoka katika harakati za kufanya  uchechemuzi wa Sheria ya Habari 1988 na Ile ya Tume ya Utangazaji ya Mwaka 1997 ili kuona vile vifungu vinavyokwanza utekelezaji wa majukumu yao ya kihabari vinaondoshwa.

Wito huo umetolewa na Afisa Programu na  Uchechemuzi wa Mapitio ya Sheria za Habari Zanzibar  kutoka Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania Zanzibar(TAMWA Zanzibar) Zaina Abdulla Mzee wakati akizungumza na waandishi wa habarialipokuwa akifungua mafunzo ya ukumbusho kwa waandashi wa habari huko katika Ofisi za Tamwa Mkanjuni Chake Chake,

Amesema umefika wakati kwa waandishi wa habari kujifunga ukaja wa kuandika habari ambazo zinazoonyesha vifungu vya sheria hizo vyenye mapungufu na madhara yake kwa tasnia ya habari visiwani hapa.

Sauti ya Afisa Programu na  Uchechemuzi wa Mapitio ya Sheria za Habari Zanzibar  kutoka Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania Zanzibar(TAMWA Zanzibar) Zaina Abdulla Mzee.

Akiwasilisha mada juu ya sheria ya Magazeti, Vitabu na Mawakala wa Habari, Sheria No. 5 ya mwaka 1988 na Sheria namba 7  ya Tume ya Utangazaji ya Mwaka 1997 na vifungu kandamizi katika sheria hiyo Mkufunzi Mshauri Haura Shamte amesema vifungu hivyo havifai kuwepo ndani ya sheria hizo.

Sauti ya Mkufunzi Mshauri Haura Shamte.

Nao Waandishi wa Habari Fatma Hamad Faki wa Blog ya Pemba ya Leo na Khadija Ali Yussuf wamebainisha baadhi ya vifungu vyenye mapungufu katika sheria na vinavyohitaji kuondoshwa.

Sauti za Waandishi wa Habari Fatma Hamad Faki wa Blog ya Pemba ya Leo na Khadija Ali Yussuf