Zenj FM

Muzdalifa yaiomba serikali kuanzisha siku ya mtoto yatima

10 December 2024, 6:54 pm

Mratibu wa Asasi  za Kiraia Mahfoudh Shaaban Haji ambae pia ni Mratibu wa Maadhimisho ya saba  ya mtoto yatima Zanzibar akizungumza na waandishi wa habari.

Na Berema Nassor.

Taasisi ya Muzdalifa Charitable Organization  Zanzibar  wameiomba  Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuweka mpango madhubuti ya kuiweka  siku ya maadhimisho ya mtoto yatima Zanzibar katika kalenda ya matukio ya kitaifa  kwa lengo la kuwatambua na kuwafariji  watoto mayatima kitaifa  hapa nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari  Katibu Mkuu wa Taasisi hiyo Farouk Hamad Khamis  katika ofisi za taasisi hiyo iliyopo amani  kuelekea  maadhimisho ya saba  ya mtoto yatima Zanzibar  amesema licha ya jitihada mbali mbali zinazochukuliwa na taasisi binafsi katika  kuhamasisha jamii juu ya kuwalea na kuwahurumia watoto hao lakini bado wanakumbana na changamoto kadhaa  za vitendo vya udhalilishaji ikiwemo kukosa haki zao za msingi kutoka kwa wazazi wao waliofariki.

Amesema taasisi hiyo ipo mstari wa mbele katika kuchukua juhudi na bidii za kuelimisha jamii juu ya kuwalea watoto mayatima katika malezi yaliyo bora.

Sauti ya Katibu Mkuu wa Taasisi hiyo Farouk Hamad Khamis.

.Kwa upande wake Mratibu wa Asasi  za Kiraia Mahfoudh Shaaban Haji ambae pia ni mratibu wa maadhimisho hayo amesema  lengo kubwa la kufanya madhimisho hayo ni kutaka kuwekwa katika kalenda ya kitaifa sambamba na kuweza kuwathamini na kuwafariji watoto mayatima hivyo kupitia tasisi hiyo imeona kwamba ni vyema kutenga siku maalum kwa ajili ikiwa ni miongoni mwa kuadhimisha siku hiyo.

Sauti ya Mratibu wa Asasi  za Kiraia Mahfoudh Shaaban Haji ambae pia ni mratibu wa maadhimisho hayo.

Kilele cha Maadhimisho ya saba ya mtoto yatima Zanzibar yanatarajiwa kufanyika tarehe 14 mwezi huu chini ya tasisi ya Muzdalifa charitable  Organization Zanzibar  ikishirikiana na wadau mbalimbali ambapo kauli mbiu ya maadimidhimisho hayo ni  KILA  MTOTO  ANASTAHIKI  KUWA  NA FAMILIA BORA.