Puma Energy yafungua Kituo cha Kwanza visiwani Zanzibar
6 December 2024, 3:25 pm
Na Berema Nassor
Waziri wa Maji Nishati na Madini Shaibu Hassan Kaduara amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kushirikiana na wadau wa sekta mbali mbali ikiwa na lengo la kuleta mabadiliko ya maendeleo ya kiuchumi katika taifa na jamii kwa ujumla.
Akizungumza na wadau wa sekta ya nishati katika uzinduzi wa kituo kipya cha mafuta melii tano fuoni Zanzibar chini ya Kampuni ya Puma Energy amesema tukio hilo linaashiria hatua nyengine muhimu katika maendeleo ya sekta ya nishati Zanzibar na uthibitisho wa ushirikiano wenye kuleta tija na mafanikio bora ya sekta binafsi ikiwemo kampuni ya Puma Energy Tanzania.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Wa Kampuni Hiyo Fatma Mohamed Abdalla amesema kituo cha kipya cha mafuta kilichopo Fuoni Zanzibar ni kituo cha kwanza kufunguliwa kisiwa Zanzibar ikiwa ni sehemu ya kuendelea kusambaza huduma za upatikanaji wa mafuta na nyenginezo katika soko la Zanzibar.
Nao baadhi ya wafanya biashara wa huduma za usafiri wa barabarani wamesema ufunguzi wa kituo hicho kitawarahisishia katika kupata huduma za mafuta ambacho kipo karibu na kituo chao cha biashara sambamba na kuweza kupata fursa za ajira kwa vijana hapa Zanzibar .
Ujenzi wa kituo hicho cha Fuoni Meli tano kimegharimu kiasi cha shilingi za Kitanzania Bilioni mbili nukta tano hadi kukamilika.