Zenj FM

Zaidi ya milioni 270 kutumika ujenzi ofisi za Jimbo Chumbuni

27 November 2024, 3:27 pm

Mwakilishi wa Jimbo la Chumbuni Miraji Khamis Kwaza akikabidhi vifaa vya ujenzi kwa Mwenyekiti wa jimbo la Chumbuni Haji Gwali Khamisi.

Na Mary Julius.

Mwakilishi wa Jimbo la Chumbuni Miraji Khamis Kwaza amekabidhi vifaa vya ujenzi wa jengo la ofisi za jimbo hilo vyenye thamani ya sh milioni ishirini na moja 21 ikiwa niutekelezaji wa ahadi zake.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo mwakilishi Miraji amesema ujenzi huo  ni sehemu ya ahadi yake ambayo ailiahidi katika kampeni za mwaka 2020 ambapo maemshukuru mwenyekiti wa jimbo la chumbuni ambaye amekuwa akimkumbusha katika kutimiza ahadi hiyo.

Mwakilishi Miraji amesema jengo hilo litakapo kamilika litasaidia jimbo kuwa na ofisi yake ili kuwaondoshea usumbufu wanachama kuwafikia viongozi.

Aidha Amesema  ujenzi wa jengo hilo unatarajia kutumia  zaidi ya shilling million 200 ambazo atatoa yeye na  ramani ya jengo hilo la ghorofa unatarajiwa kuwa na holi la mikutano  ambapo juu kutakuwa na ofisi za viongozi na jumuiya zake.

Sauti ya Mwakilishi wa Jimbo la Chumbuni Miraji Khamis Kwaza.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa jimbo la Chumbuni Haji Gwali Khamisi amesema amefurahi kwa kuanza kwa ujenzi wa ofisi hiyo kwani amepambana sana katika kuhakikisha jimbo hilo linapata ofisi yake.

Aidha amewataka wanachama wa chama cha mapinduzi kuendelea kushikamano ili kuhakikisha chama hicho kina shika madaraka 2025.

Sauti ya Mwenyekiti wa jimbo la Chumbuni Haji Gwali Khamisi

Kwa upande wake Mwakilishi wa Viti Maalum Mkoa wa Mjini Sada Ramadhani Mwendwa amempongeza Mwakilishi Miraji kwa kuweza kujenga ofisi hiyo ambapo  hapo awali walikuwa wakitangatanga kutafuta sehemu ya kufanya mikutano ya jimbo.

Sauti ya Mwakilishi wa Viti Maalum Mkoa wa Mjini Sada Ramadhani Mwendwa

 Akizungumzia uandikishaji wa wapigakura wapya ifikapo february mosi bi sada amesema viongozi wa jimbo wamejiandaa kuhakikisha vijana na wale wote ambao hawajajiandikisha katika daftari la wapigakura wana jinandikisha ili chama hicho kipate ushindi kwa kikishindo.

Sauti ya Mwakilishi wa Viti Maalum Mkoa wa Mjini Sada Ramadhani Mwendwa

Vifaa vilivyo kabidhiwa ni mchanga, nondo, kokoto na cement.