Zanzibar yaadhimisha siku ya takwimu Afrika
18 November 2024, 4:18 pm
Na Belema Suleiman Nassor
Mtakwimu mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Salum Kassim Ali amesema takwimu zinazotelewa na ofisi ya mtakwimu mkuu zinasaidia Serikali katika kupanga mipango ya maendeleo ya sekta mbali mbali hapa nchini.
Ameyasema hayo katika mkutano maalum na wandishi wa habari katika kuadhimisha Siku ya Takwimu Afrika amesema vyombo vya habari vina mchango mkubwa kwenye jamii katika kutoa taarifa za kitaakwimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa matumizi sahihi ya takwimu katika kupanga maendeleo kwa jamii na taifa kwa ujumla.
Nae Makamo Mwenyekiti wa Bodi ya Takwimu Zanzibar Mary Khatibu amesema lengo kuu la kuadhumisha siku ya takwimu Afrika ni kubadilishana mawazo pamoja na kuongeza ufahamu wa takwimu rasmi uzalishaji usambazaji na ufikiaji na utumiaji wake kwa ajili ya kufanya maamuzi na kupata ripoti kulingana na ushahidi sahihi wa kitakwimu.
Siku ya takwimu Afrika huadhimishwa kila ifikapo tarehe 18 Novemba kwa Afrika.