Zenj FM

Mwanamke Initiatives, Oryx yatua mizigo ya kuni kaya 785 Panza Pemba

13 November 2024, 6:27 pm

Mkuu wa Mkoa wa Kusini Memba Mattar Zahor Massoud akimkabidhi mmoja ya wakaazi wa Kisiwapanza Mtungi wa Gesi akiwa pamoja na Sabra Ali Mohamed Mkurugenzi Mtendaji wa MIF na Meneja wa Kampuni ya Oryx gas Zanzibar Shuwekha Omar Khamis. Picha na Is-haka Mohammed

Na Is-haka Mohammed.

Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mattar Zahor Massoud amewataka wananchi wa Kisiwapanza kutumia vyema mitungi ya gesi waliyokabidhiwa kwani imelenga kuwaondoshea changamoto za athari za kimazingira zinazoendelea kukikumba kisiwa hicho

Mattar ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Kisiwapanza kilichopo Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba katika hafla ya kukabhidhi jumla ya mitungi 785 ya gesi kwa kaya zote zilizopo katika kisiwa hicho.

Amesema lengo kubwa la kupewa mitungi hiyo ni kuweza kuitumia pamoja na kuachana na ukataji wa miti kwa ajili ya kuni na mkaa kwani zimekuwa zikisababisha athari kubwa za kimazingira na kiafya kwa wakaazi wa Kisiwapanza.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mattar Zahor Massoud.

Akizungumza katika hafla hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwanamke Initiatives Foundation Sabra Ali Mohamed amesema wanawake wa visiwa vidogo vidogo hapa Zanzibar wamekuwa wahanga wakubwa wa matumizi ya nishati isiyo safi ya kupikia pamoja na kukata miti ya mikoko.

Sauti ya Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwanamke Initiatives Foundation Sabra Ali Mohamed.

Kwa upande wake Meneja wa Kampuni ya Oryx Shuwekha Omar Khamis ameeleza athari zitokanazo na athari za utumiaji wa nishati isiyo safi kwa jamii wakiwemo wananchi wa kisiwa hicho kidogo cha Kisiwapanza.

Sauti ya Meneja wa Kampuni ya Oryx Shuwekha Omar Khamis

Wakizungumza mara baada ya kukabidhiwa mitungi hiyo baadhi ya wananchi wa Kisiwapanza wameishukuru serikali na wadau walioshirikiana nao kuwapatia mitungi hiyo na kuahidi kubadilika kwa kuwanza kutumia nishati safi na salama kwao.

Sauti wananchi.