Zenj FM

Miaka 4 ya Dk Mwinyi makusanyo ya kodi yaimarika ZRA

4 November 2024, 3:26 pm

Kaimu Kamishna Mkuu Mamlaka ya Mapato Zanzibar ZRA Said Ali Moh’d akitoa taarifa za makusanyo ya kodi  kwa  waandishi wa habari huko katika Ofisi kuu ya ZRA Gombani Chake Chake Pemba.

NA Is- haka Mohammed.

Mamlaka ya Mapato Zanzibar,ZRA imesema ongezeko la ukusanyaji wa mapato umekuwa ukiimarika kila mwaka tokea kuangia madarakani kwa Rais wa Zanzibar Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi mwaka 2020.

Akitoa taarifa ya makusanya kwa kipindi cha miaka 4 ya Rais Dkt. Mwinyi kwa waandishi wa habari huko Ofisi Kuu ya ZRA Pemba, Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Zanzibar Said Ali Moh`d amesema kuwa ongezeko hilo limetokana na kuimarishwa kwa miundombinu ya kiuchumi nchini.

Kaimu Kamishna Mkuu huyo amesema katika mwezi wa Oktoba mwaka huu ZRA idikadiriwa kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 74.549 lakini wamevunga lenga kwa kufanikiwa kukusanya jumla ya Sh bilioni 76.528 ikiwa ni sawa asilimia 102.65.

Sauti ya Kaimu Kamishna Mkuu Mamlaka ya Mapato Zanzibar ZRA Said Ali Moh’d.

Aidha amesema kuwa katika katika kipindi cha mwaka wa fedha Julai – Oktoba 2024/25 Mamlaka imeongeza makusanyo ya serikali kwa kila mwezi kwa kukusanya jumla ya bilioni 277.46 ikiwa ni sawa na bilioni 69.365 ukilinganisha na  mwisho wa mwaka wa fedha wa 2023/24 ambapo waliweza kukusanya wastani wa shilingi bilioni 59.90 kwa mwezi.

Sauti ya Kaimu Kamishna Mkuu Mamlaka ya Mapato Zanzibar ZRA Said Ali Moh’d.