Wadau wa mabadiliko ya tabia ya nchi wakutana Zanzibar
23 October 2024, 4:46 pm
Waziri wa nchi ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais Zanzibar Harusi Said Suleiman amesema serikali ya Zanzibar kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Mungano wa Tanzania zimekuwa zikichukuwa hatua mbalimbali za kuhimili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi hapa nchini ili kuondoa athari zinazotokana na hali hiyo.
Akizungumza katika mkutano wa kwanza wa mabadiliko ya tabia nchi amesema mabadiliko yatabia nchi ni janga la kitaifa ambapo nchi nyingi duniani zimeathirika na janga hilo huku Zanzibar ikiwa ni miongoni wa waathirika wa tatizo hilo.
Kwa upande wao wadau wa kongamano hilo wamesema kongamano hilo litasaidia kujenga uelewa na hamasa kwaasasi zakiraia,wanajamii na hata idara za serikali kufahamu dhana nzima ya mabadiliko ya tabia nchi na uhimili wake.
Akielezea athari za mabadiliko ya tabia nchi ambazo huwaathiri watoto Makamo Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri wa Watoto Zanzbar Muhsin Haji Simai amesema watoto hukosa kula mlo kamili kwa siku kutokana na maji chumvi kuingia katika vipando ambavyo hulimwa na wazazi wao.
Zaidi ya washiriki 250 wameshiriki mkutano huo wa kwanza wa mabadiliko ya tabia nchi kufanyika visiwani Zanzibar ambapo kauli mbiu ni IMARISHA UHIMILI WA MABADILIKO YA TABIA NCHI ZANZIBAR