Zenj FM

Chanjo ya Polio kutolewa Zanzibar baada ya miezi miwili ya kutokuwepo

22 October 2024, 3:02 pm

Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Zanzibar Dkt Salim Slim amesema Wizara ya Afya Zanzibar akitoa taarifa kwa wananchi juu ya uwepo wa chanjo.

Na Mwandishi wetu

Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Zanzibar Dkt Salim Slim amesema Wizara ya Afya Zanzibar itahakikisha inawapatia chanjo ya polio watoto wote ambao walikosa chanjo hiyo kwa kipindi cha miezi miwili iliyopita ambayo ilitokana na kutokuwepo kwa chanjo hiyo katika nchi mbali mbali za Afrika ikiwemo Tanzania.

Akitoa taarifa kwa wananchi juu ya uwepo wa chanjo hiyo amesema watahakikisha kila mtoto aliyekosa chanjo hiyo anapata kutokana na kuwa chanjo hiyo tayari ipo hapa nchini.

Amesema tatizo la ukosefu wa chanjo ya polio halikuwa la Zanzibar pekee bali tatizo hilio lilikuwepo kwa baadhi ya nchi za Afrika, sasa chanzo za polio zimeshapatikana na zoezi la utoaji wa chanjo litafanyika nyumba kwa nyumba kupitia huduma ya mkoba na vituo vya Afya vyote vya Unguja na Pemba.

Amesema Chanjo ya Polio kwa watoto husaidia kujenga kinga dhidi ya virusi vya polio husababisha ugonjwa wa polio, ambapo ni muhimu kwa kila mtoto kupata dozi 4 za chanjo hiyo.

Dkt Slim Amesema Chanjo ya polio hutolewa kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano kwa mujibu Shirika la Afya Duniani (WHO) linapendekeza dozi nyingi ili kuhakikisha kinga kamili ya mtoto dhidi ya virusi vya polio.

Sauti ya Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Zanzibar Dkt Salim Slim.

Aidha amesema kuwa ugonjwa wa polio unasababisha ulemavu kwa watoto hivyo ni vyema kila mzazi kuhakikisha mtoto wake anapata chanjo hiyo na wale ambao wanaendelea kupata chanjo hizo basi wasiache kupatiwa kwa wakati.

Sauti ya Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Zanzibar Dkt Salim Slim.