Mazrui awashauri vijana kusomea kada ya ganzi na usingizi
11 October 2024, 4:51 pm
Na Mary Julius.
Siku ya ganzi na usingizi huwazimishwa kila ifikapo tarehe 16 ya mwezi wa 10 ya kila mwaka ambapo Zanzibar itaadhimisha siku hii kwa mara ya kwanza.
Vijana wanaosoma kada ya afya wameshauriwa kutumia fursa ya kusomea kada ya ganzi na usingizi ili kukidhi hitaji la nchi kwa wataalam wa kada hiyo.
Ushauri huo umetolewa na waziri wa afya Zanzibar Nassro Ahmed Mazrui alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya siku ya ganzi na usingizi dunia ambapo amesema Zanzibar bado inakabiliwa na uhaba wa taalamu hao.
Amesema kada ya ganzi na usingizi bado inahitaji wataalamu kutokana na umuhimu wake katika sekta ya afya nchini na serikali ya mapinduzi Zanzibar imejidhatiti kuwasomesha wataalamu hao na kuwawekea mazingira mazuri pamoja na maslahi yo.
Hata hivyo waziri Mazrui amesema kuwa milango ya wizara ipo wazi kuwapa ushauri vijana wanaotaka kujiendeleza katika taaluma ili waweze kuchagua kada hiyo ya ganzi na usingizi.
Amesema Zanzibar ina wataalam bingwa wa ganzi na usingizi wane,wataalamu wa ngazi ya shahada ya kwanza 2 na ngazi nyengine 18 unguja na pemba ambao wanatengeneza idadi ya wataalamu 49.