Mpango mkakati wa miaka 5 uendane na uimarishaji huduma bora kwa jamii
8 October 2024, 4:40 pm
Na Mary Julius.
Mkuu wa Mkoa Kusini Unguja Ayoub Mohd Mahmoud, amewataka viongozi na watendaji wa baraza la mji kati Kuhakikisha mpango mkakati wa miaka mitano wanao uandaa unalenga uimarishaji wa huduma Bora kwa jamii na unakidhi mahitaji ya wananchi.
Ayoub ameyaeleza hayo huko Dunga ukumbi wa baraza la mji kati wakati akizungumza na madiwani, viongozi kutoka benki ya NMB na PBZ pamoja na watendaji wa baraza hilo katika kikao cha mapitio ya rasimu ya utaarishaji wa mpango mkakati wa miaka mitano unaoanzia 2025/2030.
Amesema watendaji wanapaswa kutambua kwamba ili mpango huo unaoandaliwa uweze kutekelezekaipasavyo unahitaji kupata maoni ya wananchi kulingana na wakati wa sasa na wa baadae pamoja na usimamizi mzuri wa ukusanyaji wa mapato na utunzaji wa raslimali kwani nchi nyingi duniani mabaraza na manispaa yameweza kupiga hatua kubwa za maendeleo kutokana na utaratibu huo
Aidha amewasisitiza watendaji hao kuendelea kuongeza kasi ya uwajibikaji ili kuliongezea hadhi baraza hilo liweze kupanda kutoka baraza la mji Kwenda manispaaa.
Mkurugenzi wa Baraza la mji kati Salum Mohd AbubKar amesema mpango huo wa miaka mitano umelenga kushirikisha jamii katika nyanja mbali mbali za kiuchumi ikiwemo utunzaji wa rasimali, uchumi Wa bluu, usafi wa mazingira, pamoja na kuweka mipango miji ilio Bora.
Kwa upande wake Mshauri Elekezi kutoka Dar-es-saalam Dk Pauline Mtunda amesema kutokana na mpango huo ni vyema kwa Baraza hilo kuwa na mipango madhubuti ya ukusanyaji na matumizi ya mapato yatokanayo kodi za wananchi kuona zinarudi kuwanufaisha kupitia miradi ya maendeleo.