Zenj FM

UWT Zanzibar watakiwa kujiandikisha daftari la kudumu la mpiga kura

8 October 2024, 2:26 pm

Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Maghribi kichama Tauhida Galos Nyimbo, akizungumza na Wananchi wakati alipofanya ziara ya kukaguwa vituo vya undikishaji wa Daftari la kudumi la wapiga kura  katika Wilaya ya Dimani kichama.

Na Mary Julius

Mbunge wa Viti maalum Mkoa wa Magharibi kichama Tauhida Galos Nyimbo amewataka Wanachama wa UWT kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika Daftari la kudumu la wapiga kura linaloendelea.

Tauhida ameyasema hayo wakati alipofanya ziara ya kukaguwa zoezi la uandikishaji wa Daftari la kudumu la mpiga kura katika Mkoa wa Magharibi kichama.

Amesema mtaji wa vyama siasa ni kuwa idadi kubwa ya wapiga kura hivyo iwapo watajitokeza kwa wingi kujiandikisha katika Daftari la kudumu la Wapiga kura, itawawezesha kukipatia ushindi chama hicho, ifikapo mwaka 2025.

Aidha amewataka Vijana hao kuhamasishana ili wapate kufanya maamuzi sahihi ya kuchaguwa au kuchaguliwa katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika hapo mwakani.

Mbunge wa maalum Mkoa wa Maghribi kichama Tauhida Galos Nyimbo, akizungumza na Wananchi wakati alipofanya ziara ya kukaguwa vituo vya undikishaji wa Daftari la kudumi la wapiga kura  katika Wilaya ya Dimani kichama.

Kwa upande wake Msimamizi wa Daftari la kudumu la Wapiga kura katika Jimbo la Mwera Salama Khamis Suleiman amesema zoezi hilo limeenda vizuri na kuwaomba Wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika Daftari hilo.

Hata hivyo amefurahishwa na idadi kubwa ya Wananchi waliojitokeza kujiandikisha katika Daftari la kudumu la kupiga kura jambo ambalo litapelekea Vijana kupata haki yao ya msingi ya kuchaguwa na kuchaguliwa.