Zenj FM

Vijana jitokezeni kugombea nafasi za uongozi CUF Zanzibar

25 September 2024, 6:31 pm

Picha ya makao mkuu ya chama cha Wananchi CUF Mtendeni Zanzibar

Na Khalida Abdulrahman

Chama cha Wananchi CUF kimewataka vijana kujitokeza kwa wingi katika kugombea nafasi mbalimbali ndani ya chama hicho.

Akizungumza na Zenj FM Mkurugenzi wa Itifaki na Udhibiti wa Chama Cha Wananchi CUF Taifa Rajab Mbarouk Mohd akiwaa  makao makuu ya chama cha wananchi CUF Mtendeni Wilaya ya Mjini amesema kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025 chama hicho kimejipanga kufanya uchaguzi wa ndani utakao wavusha katika kipindi cha uchaguzi mkuu ujao.

Mkurugenzi amesema mpaka sasa chama hicho kimepokea form za watiania 8 kwa kwajili ya nafasi ya mwenyekiti, na kwa upande wa makamu mwenyekiti chama kimepokea maombi 12 kwa Tanzania bara na Zanzibar.

Aidha amesema chama kinatoa fursa mbali mbali kwa wanawake na vijana ili kujitokeza kwa wingi  katika kugombea nafasi  mbali mbali za uongozi ikiwemo katika jumuiya za kinamama ,jumuiya za vijana na nafasi nyengine za chama.

Akizungumzia uchaguzi wa serikali za mitaaa mkurugenzi amesema chama hicho kimejipanga kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa kwani  asilimia 95 kwa vijiji vyote na mitaaa yote.

Mkurugenzi wa Itifaki na Udhibiti wa Chama Cha Wananchi CUF Taifa Rajab Mbarouk Mohd.

Naye Naibu Katibu Mtendaji Jumuiya Vijana Taifa Khadija Salim Aliy amesema kutoa fursa kwa vijana kugombea katika nafasi mbali mbali za kichama ni haki ya kikatiba kila mtu kugombea nafasi anayoitaka kwanzia ngazi za matawi mpaka taifa.

Sauti ya Naibu Katibu Mtendaji Jumuiya Vijana Taifa Khadija Salim Aliy