Wanafunzi Zanzibar washauriwa kujiwekea malengo
21 September 2024, 3:38 pm
Na Mwandishi wetu.
Wanafunzi Zanzibar wameshuriwa kujiwekea malengo ya kitaaluma mara baada ya kumaliza elimu sambamba na kuwa ushirikiano ili kujenga jamii iliyo bora.
Ushauri huo umetolewa na Mwanariadha wa Kimataifa wa Grenad, Lindon Victor, alipokuwa akizungumza na wanamichezo wa Sekondari ya Ben Bella na Haile Salassie.
Amesema, ni muhimu kwa wanafunzi hao kujipangia mustakbali wa maisha yao ya ya badae na kuzingatia ushauri wa watu wenye malengo ya maendeleo na kuacha kushirikiana na watu wenye mitazamo iliyokosa malengo.
Amesema, wanafunzi wanapokuwa wameweka malengo iwe ya kimasomo au kimichezo wanakuwa wametengeneza hatma bora kwa ajili ya maisha yao ya baadaye.
“Kwa dunia ya sasa elimu ndiyo kila kitu, lakini, msisahau michezo nayo ina fursa nyingi ya kufanikiwa kimaisha.
“Kati yetu wapo wanafunzi ambao hawatobahatika kuendelea na elimu ya juu zaidi, lakini, michezo pia ina sehemu kubwa ya maisha bora”, alisema, mshindi huyo wa medali ya dhahabu ya michezo ya Olimpiki ya Paris 2024.
Aidha Mwanaridha huyo amewatolea mfano wa yeye mwenye ambapo amesema, alikulia katika familia masikini, lakini, michezo ndiyo iliyomuondoa kwenye umasikini huo na sasa akiwa na jina kubwa duniani.
“Wazee wangu walikuwa masikini na mimi niliishia nikiwa nachunga mifugo, lakini, niliweka malengo ambayo yameniwesha kufika hapa nilipo sasa”.
Kwa upande wake Rais Waziri wa Michezo wa Sekondari ya Haile Salassie, Ally Abdul Ally, amewashauri wanafunzi wenzake kuendeleza mashirikiano baina yao na walimu ili kufikia malengo yao waliyojiwekea iwe ya kielimu au kimichezo.