Zenj FM

Mafunzo ya Amali fursa kwa vijana kujiajiri

19 September 2024, 5:25 pm

Banda la Kituo cha Elimu Mbadala katika maonyesho ya Mafunzo ya Amali Kisonge,

Na Khalida Abdulrahman.

Vijana wameshauriwa kujiunga na vituo mbali mbali vya Mafunzo ya Amali ikiwemo mafunzo ya ufundi upishi  na uchoraji ili kujiajiri wenyewe.

Akizunguimza na Zenji Fm Mwalimu wa skuli ya forodhani Sunskim Mwajuma Mussa Said akiwa katika maonyesho ya mafunzo ya amali katika viwanja vya Mnarani Kisonge Wilaya ya Mjini,amesema vijana na watuazima wanaopenda kujifunza elimu mbaadala wanatakiwa  kutumia fursa kwa kujiunga na vituo hivo vya mafunzo ya amali ili kuwa na ujuzi tofauti    ikiwemo kushona kudarizi pamoja na kupika.

Aidha mwalimu amewataka wazazi kuacha kuwachagulia fani za ujuzi  watoto badala yake waawache watoto wasomee fani wanazo zitaka.

Sauti ya Mwalimu wa skuli ya forodhani Sunskim Mwajuma Mussa Said

Nae Mwanafunzi Hidaya Ali Mohd anayesoma elimu mbadala amewashauri vijana waliokata  tamaa  wajiunga na elimu mbadala ili kufikia malengo  na kujikwamua kiuchumi.

Sauti ya Mwanafunzi Hidaya Ali Mohd