Wafanyabiashara Kwarara walia na ucheleweshwaji wa uzoaji wa taka
19 September 2024, 4:49 pm
Na Khaira Ame Haji.
Katika kuhakikisha Wafanyabiashara wa maduka ya Kwarara Wilaya ya Magharibi B wanafanya biashara katika hali ya usafi wameliomba Baraza la Manispaa Magharib b kuchukua taka kwa wakati.
Wakizungumza na Zenj Fm wafanyabiashara hao amesema pamoja na kutozwa ada ya taka ya shilingi elfu hamsini (50) kwa mwaka lakini bado taka zinazagaa katika maeneo yao ya biashara hali inayo pelekea kutafuta njia nyingine ya kuziondoa taka hizo na kuongeza gharama ya uendeshaji wa biashara katika maeneo hayo.
Aidha wameliomba Baraza la Manispaa kushirikiana na wafanyabiashara kupita kuchukuwa taka mara kwa mara ili kuboresha mazingira ya biashara na kuhakikisha kuwa taka zinatupwa sehemu sahihi.
Kwa upande wake Mhasibu Mapato kutoka Baraza la Manispaa Magharibi B Naila Khamisi Ali amesema jukumu la usafi ni la kila mtu na wafanyabiashara wana wajibu wa kuchangia fedha hiyo ili kuweka mji safi.