Wananchi watakiwa kujitokeza kuchunguza saratani Zanzibar
19 September 2024, 3:51 pm
Na Mary Julius.
Kwa mujibu wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road asilimia 80 ya wagonjwa wanaotoka Zanzibar huwa wanafika hospitalini hapo wakiwa na saratani stage 4 ambayo ni ngumu kutibika jambo linalochangia vifo vya mapema.
Wananchi wa Zanzibar wametakiwa kujitokeza kwa wingi Kwenye zoezi la uchunguzi na matibabu ya saratani za aina Mbalimbali liloanza leo katika viwanja vya kiwanja cha stela Shehia ya Uholanzi Wilaya ya Magharibi A.
Wito huo umetolewa na Meneja Kitengo cha Maradhi Yasioambukiza Zanzibar Dkt Omar Mohemed Suleiman, amesema zoezi hilo la upimaji wa saratani ni la bure Kwa wananchi wote hivyo ni muhimu wa wananchi Kujitokeza ili kuweza kubaini viashiria vya saratani ili Waweze kupatiwa matibabu.
Amesema lengo la zoezi hili ni kubaini hali ya saratani Zanzibar na kupata takwimu sahihi ya watu Wanaosumbuliwana ugonjwa huo ili serikali iweze kupanga Mikakati bora ya kukabiliana na ugonjwa wa saratani.
Nae Daktari Bingwa wa Saratani Kutoka Taasisi ya Saratani ya Ocean Road Dkt Nuru Mlagalila amesema kuwa zoezi hilo Litafika katika wialaya zote za zanzibar na kwasasa Wameanzia Magharibi A.
Amesema iwapo mtu atagundulika na dalili za saratani Atapatiwa matibabu katika hospitali zetu za ndani na iwapo Itahitajika kusafirishwa ataenda kupatiwa matibabu katika Taasisi ya saratani ya ocean road bila malipo.
Kwa upande wake Katibu Tawala Wilaya Ya Magharibi A Juma Abdallah Hamad zoezi hili litafanyika katika shehia saba ndani ya wilaya ya magharibi a na kuwataka wananchi kutumia fursa hiyo kupima na kuanza matibabu mapema iwapo atagundulika na viashiria vya saratani.
Sheha wa shehia ya uholanzi na baadhi ya wananchi Waliojitokeza katika zoezi hilo wamewaomba wananchi kutumi siku hizo saba za zoezi la upimaji wa saratani kupima afya zao.