Zenj FM

Hati za haki ya matumizi ya ardhi, kilimo mwarobaini migogoro ya ardhi Zanzibar

17 September 2024, 7:56 pm

Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Rahma Kassm Aliy akikabidhi hati za Haki ya matumizi ya ardhi na kilimo  kwa mwananchi, hafla ilo fanyika  kikwajuni Zanzibar.

Wanachi wametakiwa kufuata utaratibu ulio wekwa na kamisheni ya ardhi ili kupata vibali na kuondokana na migogoro ya ardhi.

Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Rahma Kassm Aliy ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa utoaji  wa hati za Haki ya matumizi ya ardhi na kilimo  hafla ilo fanyika  kikwajuni Zanzibar.

Aidha Waziri Rahma amewataka wanachi   kufuata taratibu za kisheria zilizowekwa na mamlaka husika  ili kuweza kuepusha migogoro Mbali Mbali inayoweza kujitokeza baina Yao pamoja na kupatiwa nyaraka zinazotambuliwa na serikali. 

Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Rahma Kassm Aliy.

Nae Katibu Mtendaji kutoka Kamisheni ya Ardhi Mussa Kombo Bakari amesema ni vyema jamii ikaendeleza na kukuza Mashamba ili yaweze kudumu Kwa vizazi  vya sasa na vijavyo.   

Sauti ya Katibu Mtendaji kutoka Kamisheni ya Ardhi Mussa Kombo Bakari

Akizungumza Kwa niaba ya wananchi wezake waliopatiwa hati miliki za ardhi za kilimo  wanaishukuru serikali Kwa kuwapatia nyaraka hizo kwani kumepunguza changamoto Mbali mbalimbali ambazo zilikuwa zikiwakabili.

Sauti Mwananchi.