Zenj FM

Bidhaa zilizokwishwa muda wa matumizi zakamatwa madukani Zanzibar

13 September 2024, 5:21 pm

Baadhi ya bidhaa zilizoisha muda wa matumizi zilizokamatwa.

Na Mwanamiraji Abdallah

ZFDA imetoa wito kwa wafanyabishara kufuata sheria na kuacha tabia ya kuuza bidhaa zilizoisha muda wake kwani jambo hilo hupelekea athari kwa watumiaji.

Wakala wa Chakula, Dawa na Vipodozi ZFDA Zanzibar kwa kushirikiana na Jeshi na Polisi na Uhamiaji wamefanikiwa kukamata bidhaa za vyakula  na vipodozi  zilizoisha muda wa matumizi katika maduka mbalimbali ya mjini.

Bidhaa hizo zilizokamatwa ni pamoja na mafuta tani 1, bia ,maharage ya makopo, mahindi ya makopo, sweet cone, maziwa ya maji, tambi vilivyopatikana katika ghala la kampuni ya Cross Border Trading Company Limited lililopo Tomondo pamoja na sabuni na vipodozi vilivyopatikana katika maduka ya darajani.

Mkurugenzi Idara ya Udhibiti Usalama wa Chakula na Ufanisi Dkt. Khamis Ali Omar akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mombasa Wilaya ya Magharib B.

Akitoa taarifa ya ukaguzi walioufanya ZFDA Mkurugenzi Idara ya Udhibiti Usalama aa Chakula na Ufanisi Dkt. Khamis Ali Omar amesema katika ukaguzi huo wamebaini kuwa kuna baadhi ya wafanyabiashara hawafuati sheria na taratibu zilizowekwa kwani katika ghala hilo na maduka hayo bidhaa nyingi zimeisha muda wake.

Sauti ya Mkurugenzi Idara ya Udhibiti Usalama wa Chakula na Ufanisi Dkt. Khamis Ali Omar